Idara ya Afya imeendelea kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa lengo la kuboresha huduma za Afya za wananchi,Ikiwa ni pamoja na Tiba,Kinga,Elimu ya Afya na kujenga uwezo ili kuhakikisha huduma inayotolewa inakuwa ya kiwango cha juu na kuimarisha Afya ya Jamii.
Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ina jumla ya Kaya 49817, Kulingana na Sera na Miongozo ya Uchangiaji wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii,Asilimia 30% sawa na Kaya 14,946 zinatakiwa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii.
Jumla ya kaya zote katika Wilaya ya Kyerwa zilizojiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ni takribani 688 sawa na asilimia 4.6% ya Kaya zote zinazotakiwa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ya Jamii kwa mwaka 2015.
Vituo vya kutolea huduma za afya
Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa inasimamia vituo vya kutolea huduma vipatavyo (32).Katika kuboresha nakusogeza huduma za Afya kwa wananchi Wilayani Kyerwa,Tumefungua Zahanati sita ambazo ni Kihinda,Karongo na Rukuraijo,Rwenkende,Bugara na Karongo zote kwa pamoja zimeanza kutoa huduma kuanzia mwishoni mwa mwezi wa nne mwaka 2014.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved