Wilaya ya Kyerwa ina jumla ya vijiji 93.Vijiji 36 vimepimwa na vina vyeti (Village Certificate). Asilimia kubwa ya wakazi wa Wilaya hii wanaishi katika maeneo ambayo hayajapimwa.Shughuli za matumizi bora ya ardhi bado hazijafanyika kwa kiwango kikubwa kwa kufuata sheria,kanuni,na taratibu za uendelezaji wa ardhi.
Idara hii inasimamia na kutekeleza sera ya ardhi ya mwaka 1995 pamoja na sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na sheria ya Ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999, Sheria ya Mipangomiji Na.8 ya mwaka 2007, aidha kitengo cha Maliasili kinasimamia utekelezaji wa sera ya Taifa ya misitu ya mwaka 1998 na sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002,sera ya Taifa ya ufugaji nyuki ya mwaka 1998 na sheria ya nyuki namba 15 ya mwaka 2002 na sera ya wanyamapori ya mwaka1998 na sheria ya wanyamapori namba 16 ya mwaka 2002.
Usimamizi wa matumizi bora ya ardhi vijijini na hifadhi ya mazingira inapaswa kufanywa kwa kutumia sera na sheria za ardhi na misitu ili kuwa endelevu na wenye manufaa kwa rasilimali za nchi.
Upimaji Ramani
Kitengo hiki kinashughulika na uuandaaji wa ramani pamoja na kupima mashamba na viwanja i lengo ikiwa ni kutekeleza sera ya ardhi ya kuwapatia wananchi makazi bora.
Halmashauri kwa sasa imeshaandaa michoro ya Mipangomiji katika eneo la makao makuu ya Wilaya (Rubwera) na kupima jumla ya viwanja 1255 vya matumizi ya makazi,Biashara, Makazi/biashara, Viwanda,Taasisi pamoja na viwanja vya Matumizi ya Umma.
Uthamini wa ardhi
Halmashauri imekuwa ikithaminisha ardhi pale inapobidi ili kutoa haki kwa wananchi wakati wa fidia ili kupisha miradi ya maendeleo kutekelezwa katika Wilaya.Pia imekuwa ikitoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi pale wanapokuwa wakihitaji huduma za uthamini wa ardhi zao kwa madhumuni tofautitofauti.
Wanyamapori na Misitu
Halmashauri imekuwa ikitoa Elimu kuhusu uhifadhi wa mazingira.Kupitia elimu hiyo uhifadhi wa vyanzo vya maji umekuwa ukifanyika kwa kupanda miti rafiki ya mazingira kama mitoma(Ficus spp) na mikuyu (Ficus thoringii).Kupitia elimu hii pamoja na uhamasishaji, wadau wengi kwa sasa wanayo mashamba yao ya kupandwa hivyo kupunguza wimbi la ukataji wa miti ya asili.
Pia Wilaya ya Kyerwa ina mapori mawili ya akiba ya wanyamapori.Mapori hayo ni pamoja na Rumanyika Orugundu,na Ibanda.Mbuga hizi zina wanyama wengi kama vile Pofu,Nyemera,Mamba,Viboko,Twiga,Simba,Kuro,Nyati,Tembo,na Ndege wa aina mbalimbali.Mapori haya ya akiba mbali na kuwa kivutio kwa Watalii na Wananchi wanaopenda kuangalia wanyamapori,mito na mabonde,vilevile hutumika kwa shughuli za uwindaji wa kitalii.Taarifa kutoka kwa wawindaji bingwa pamoja na menejimenti ya Pori la Akiba Ibanda inaonesha kuwa kuna densite kubwa ya chui kwenye Pori la Ibanda ikilinganishwa na mapori mengine ya Akiba hapa nchini.
Nyuki
Ufugaji wa Nyuki katika Wilaya ya Kyerwa unaendeshwa kwa njia ya kiasili.Hata hivyo Halmashauri inaendelea kutoa elimu juu ya ufugaji wa Nyuki kwa kutumia mizinga ya Kisasa katika Kata za Rukuraijo na Rutunguru.
Wafugaji wamekuwa wakihamasishwa kujiunga kwenye vikundi vidogo vidogo vya ufugaji nyuki ili wawezeshwe kupata misaada na mikopo kwa urahisi na hivyo kujiongezea kipato.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved