Wilaya ina hekta 162,000 ambazo zinafaa kwa Kilimo, hekta 83,270.5 ndizo zinalimwa kwa sasa. Mazao yanayozalishwa kwa wingi ni pamoja na Ndizi, Maharage, Mahindi, Viazi vitamu, Viazi Mviringo, Ulezi, Mtama, Uwele, na Kahawa.
Mazao makuu ya Chakula ni Ndizi, Mahindi, Maharage, na Viazi ambapo Kahawa, Mtama, na Ndizi Kali ni mazao ya Biashara. Kilimo kinakisiwa kuchangia 75% kwenye pato la Wilaya. Wananchi 85% wamejiajiri kwenye shughuli za kilimo.
Umwagiliaji
Kwa sasa Kilimo cha Umwagiliaji kinafanyika sehemu chache sana na kwa wakulima baadhi tu. Kwa kuliona hili tatizo Halmashauri kupitia idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika imeandaa andiko la mradi "District Investment Profile" ambalo limeainisha maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa Kilimo Cha Umwagiliaji. Maeneo/Vijiji/Kata yaliyopo kwenye mpango wa matumizi haya ni pamoja na Ziwa Karenge, Ziwa Rushwa, Ziwa Rwere-Nkwenda, Mto Kagera, Safu za milima ya Kyerwa, na Bonde na Sina.
Hali ya chakula
Hali ya Chakula Wilaya ya Kyerwa kwa sasa inaridhisha kutokana na wakazi wanaostahili kuwepo. Kiasi kinachozalishwa kwa sasa kingekuwa zaidi endapo kusingelikuwepo na ugonjwa wa Mnyauko unaoshambulia zao la Mgomba (Unyangano).
Matumizi ya zana za Kilimo
Wilaya kwa sasa haina Matrekta ya kutosha kwa ajili ya Kilimo hivyo kufanya wakulima walio wengi kutumia jembe la mkono. Katika kulikabiri hili Wilaya imeelekeza jitihada za makusudi kuwahamasisha wakulima binafsi kujikita katika ulimaji wa kutumia wanyama kazi kama Ng'ombe wa maskai na jembe la Plau. Pia Halmashauri inahamasisha wakulima kujiunga katika Vikundi ili kujenga mazingira mazuri ya kupata mkopo nafuu wa Matrekta kupitia SUMA JKT.
Juhudi za Halmashauri katika kuendeleza sekta ya Kilimo
Kutokana na Kilimo kuwa tegemeo la kiuchumi kwa wananchi waliowengi Wilayani Kyerwa, Serikali kupitia Halmashauri imejipanga kuboresha yafuatayo ili kuinua uzalishaji wa mazao ya kilimo:-
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved