Mkuu wa wilaya ya kyerwa Mhe. Zaituni Msofe amewataka Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na Serikali katika kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Mpox katika maeneo yao.
Ameyasema hayo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa wakati akitoa maelekezo ya Serikali katika kikao cha baraza la madiwani lililofonyika 22 Agosti 2024 kwa ajili ya kujadili taarifa utekelezaji kwa robo ya nne ya Aprili hadi Juni 2023/2024.
Mhe. Msofe amesema Serikali kupitia Idara ya Afya inatakiwa kuendelea kuweka mikakati ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu tahadhari na kinga ya ugonjwa wa Mpox ili waweze kujua namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Aidha Mkuu wa Wilaya amesema licha ya kwamba ugonjwa huo haujatangazwa kuingia nchini lakini ni vizuri wananchi kupatiwa elimu namna bora ya kujilinda kuhusu ugonjwa huo na kuanza kuchukua tahadhari.
Vile vile Mkuu wa Wilaya amekabidhi Vishikwambi kwa Waheshimiwa Madiwani ambavyo vimenunuliwa kwa mapato ya ndani ya halmashauri ili kuachana na matumizi makubwa ya karatasi na kuokoa gharama za usambazaji wa makabrasha na hivyo kuwezesha vikao kuendeshwa kidigitali.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved