Kamati ya fedha na uongozi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Bahati Henerico imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo katika Kata za Rukuraijo, Kikukuru na Nkwenda.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na kitalu cha kuotesha Miche ya Kahawa chenye miche 1,600,000 ambao unamilikiwa na Ndg. Singsibert Kashunju kwa ufadhili wa Bodi ya Kahawa (TCB) chini ya usimalizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa. Ukugauzi wa eneo la ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari ya Rwere ambayo itaanza kujengwa kwa nguvu za wananchi hadi kufikia sasa wamekusanya mawe, michanga na kuchanga fedha taslimu Tsh.23,470,000/= na wanatarajia kuanza ujenzi muda wowote.
Kutembelea ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vyenye thamani ya Tsh.75,000,000/= katika shule ya Sekondari Mukire ambayo yamekamilika kwa asilimia mia, pamoja na kuwapongeza Walimu wa shule hiyo kwa ufaulu bora wa matokeo ya kidato cha sita ambao wanafunzi wote walipata daraja la kwanza na shule hiyo kuwa ya kwanza kiwilaya na ya 35 kitaifa. Pia Kamati imekagua ujenzi wa vyumba 10 vya maduka katika stendi ya Nkwenda ambao uko katika hatua ya umaliziaji.
Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa miradi yote ambayo imeitembelea na kuikagua huku ikitoa maelekezo mbalimbali kwa kila mradi ili kuleta tija kwa umma na kuzidi kusisitiza uadilifu katika matumizi ya fedha za serikali kwa miradi inayoendelea na kuwataka wataalam kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved