Mafunzo ya uandikishaji orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kuanza tarehe 11 hadi 20 Oktoba 2024 yamefanyika leo tarehe 7 Oktoba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Kyerwa Modern ambapo maafisa wandikishaji wamepatiwa mafunzo ya uandikishaji wa wapiga kura kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni.
Mjumbe wa kamati ya uchaguzi mkoa wa Kagera Adv. Jovin Rutainulwa ambaye alimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Kagera amewataka maafisa wandikishaji wa orodha ya wapiga kura wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kwenda kutekeleza jukumu lao kwa Uaminifu na uadilifu.
Naye Ndugu Msafiri Mayunga akimuwakilisha Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa amewataka washiriki wa mafunzo hayo kwenda kuishi kiapo chao ambacho wamekitoa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Allen Ifunya katika utekelezaji wa majukumu yao ya uandikishaji katika vituo vyao.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved