Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Mhe. Zaituni Msofe ametoa rai kwa wananchi wa Kata ya Nkwenda wilayani hapa kwenda kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, ili waweze kumchagua kiongozi bora atakayewaletea maendeleo katika vijiji na vitongoji vyao.
Mheshimiwa Msofe ametoa rai hiyo, leo tarehe 18 Oktoba 2024 alipotembelea Kata ya Nkwenda na kuzungumza na vijana wa Bodaboda na wajasiriamali kwa lengo la kutoa hamasa kwa Vijana wa Kata hiyo kushiriki kikamilifu katika zoezi linaloendelea la kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura na kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ajili ya kumchagua kiongozi bora ifikapo 27 Novemba 2024
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved