Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ikiambatana na wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa imefanya ziara ya kukagua na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya ya Kyerwa leo 30 Oktoba 2024 kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi hiyo.
Katika ziara hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Mhe. Bahati Henerico imekagua na kutembelea miradi mitano Ujenzi wa wa Shule ya Sekondari Shikizi Umoja -Rwabwere, Shule ya Sekondari Shikizi ya Nyarutuntu-Nkwenda, Shule Msingi Shikizi ya Ihanda-Nyakatuntu, Ujenzi wa Wodi ya Magonjwa Mchanganyiko katika kituo cha afya Nkwenda-Nkwenda na eneo la Ujenzi wa Shule ya Mchepuo wa Kiingereza itakayojengwa katika kijiji cha Kyerwa Kata ya Kyerwa.
“Tunatembelea miradi inayoanzishwa hasa hii ya Shule zetu shikizi ambazo zimeanzishwa na wananchi na kuchangiwa na Serikali, ili tukienda kwenye vikao tuone namna ya kuzijengea hoja ili zipatiwe fedha na ziweze kusajiliwa na kukamishwa ili ziendelee kuwasaidia watoto wetu” ameeleza Mhe. Bahati.
Kyerwa District Council
Anuani ya Posta: P.O Box 72, KYERWA
Simu ya mezani: +255 686 397 972
Simu ya Mkononi: +255 754 422 746
Barua pepe : ded@kyerwadc.go.tz
Hakimiliki©2017 GWF, Kyerwa District Council. All Rights Reserved